Mwaka huu unatakiwa uwe ni mwaka wa mafanikio kwetu sote. Ila pia mafanikio hayaji bila malengo. Na malengo nayo hayafikiki bila kuekeza. Kwa kutafakari hilo leo nikaona tuanze mchezo wa kuhamasishana kuekeza. Unachohitaji kufanya ni mambo matano tu ili uweze kuekeza fedha zitakazo kusaidia kufikia malengo yako. 1. Weka Malengo - Hakikisha unajua una malengo gani na kuyafikia malengo hayo unahitaji muda gani. 2. Andaa Bajet - Pia ni vizuri kujua bajaeti yako kwa kwa wiki au mwezi, upate kujua matumizi yako ni kiasi gani na kipato ulichonacho kisha amua utakua anahifadhi pesa kiasi gani 3. Epuka Gharama za ziada - Jitahidi sana kuepuka gharama zisizo za lazima ili uweze kuekeza kama ulivyotamani kuekeza kwa wiki, au kwa mwezi n.k 4. Punguza bili za mwezi - Wote tunajua kuna gharama za lazima ambazo hazikwepeki kama Pango, maji, umeme, maziwa n.k. Gharama hizi ni za lazima ili ukijibana ndani ya budget inaweza kukusaidia kuekeza kwa mujibu wa malengo yako. 5. Fungua Account yenye gh